Tuesday 19 April 2016

Zijue Ujuzi na tabia ya mwanafunzi


Wakati wanafunzi hawawezi kujifunza na vifaa vilivyokamilika-vitabu, filamu, ao video vya kuangalia kwa macho, vitu vya kuchezea, tepu au mihadhara ya kusikiliza; michezo mingi ya viungo-hawafanikishi wanachu-ohitaji kufanikisha. Utafiti umeshafumbua umuhimu wa kurekebesha mbinu mbalimbali za kujifunza kulingana na mtindo wanafunzi wanaoutumia kujifunza. Kwa kuongezea, ukaribu wa kupatana wa mtindo wa wanafunzi wa kujifunza, ndipo wanapofanya vizuri na kupata alama za wastani (Dunn, R., Griggs, Olson, Gorman, & Beasley, 1995).
R. Dunn na K. Dunn (1992) wamefumbua kuwa faida ya modeli ya mbinu za kujifunza unaoeleweka kwa sababu sio tu watu wengi wanaathiriwa na mitindo ya kujifunza, buli vipengele vingi vya kujifunza ni maarufu katika kuongeza uwezo wa kufaulu kimasomo. R. Dunn na Griggs (1995) alianzisha modeli ya mtindo wa kujifunza unaofumbua kuwa wanafunzi wanadhuriwa na vigezo vitano:
Mazingira yao ya karibu (souti, mwanga, joto, na vifaa kama dawati/ mazingira yaliyoundwa.
Muhemuko wao wenyewe (motisha, shilizo, uwajibikaji, nafasi ya kufanya vitu jinsi wanavyopenda)
Uchguzi wao wa kijamii (kujifunza peke yao na katika saizi mbali mbali za vikundi)
Tabia yao ya kisaikolojia (uwezo uliodumishwa na usikivu, kuona, maumbile, na tabia ya mipangilio)
Mwelekeo wa njia za kujifunza (ujumla/ kwa kuchanganua, kulia/kushoto, kwa msukumo/ kwa kufikiria) (Dunn & Dunn, 1995).
Maelezo zaidi yanaonyesha ni kwa namna gani kujifunza kwa wanafunzi kunaweza kukaathiriwa na vigezo hivi vitano na vipenglele vyake. Kuhusu mazingira yao ya karibu, ingawaje wanafunzi wengi wanahitaji wakati wa utulivu wanvyokuwa wakijifunza habari kwa makini, wengine wanajifunza vizuri kukiwa na makelee kuliko kukiwa hakuna (Pizzo, imenukuriwa katika Dunn, R. Na Dunn, K., 1989). Kwa kuongezea, wakati wanafunzi wengine wanaelewa vizuri kwenye vyumba vyenye mwanga, wengine wanjifunza vizuri kwenye vyumba vyenye mwanga laini. Mwanga wa taa ya mshumaa huwachangamsha baadhi ya wanafunzi na kusababisha kuwa na wasiwasi katika shughuli na hali ya kutokutulia (Dunn, R., Dunn, K., Price, 1989).
Vigezo vingine vya kimazingira vinavyoweza kuathiri kujifunza ni pamoja na joto, na jinsi muundo wa fanicha. Wanafunzi wengine hufaulu vizuri katika mazingira yenye joto na wengine kwenye mazingira yenye baridi (Hart, 1981). Watu wengine wanapendelea kusoma katika sehemu za miti, mipira, na viti vya chuma, wengine huwa hawapendelei kusoma katika mazingira yenye viti vya kisasa ambavyo vinawazuia kusoma.
Mihumuko ya wanafunzi wenyewe inaweza pia ikaathiri uwezo wao wa kujifunza. Motisha yao ya ndani, kuvumilia na kumaliza kazi, uwezo wa kuwajibika katika tabia zao na kazi, au nafasi ya kufanya vitu kwa njia zao wenyewe vyote vinaweza vikawa ni vigezo vinavyoweza kumfanya mwanafunzi aweze kujifunza kwa njia nyingi tofauti (Dunn, R. & Dunn, K., 1989).
Vigezo vya kijamii vinaweza vika athiri kujifunza. Mwalimu anahitaji kuwa anaelewa jinsi wanafunzi wanavyojifunza katika mazingira mbalimbali. Mambo yanayoweza kuppinga kujifunza ni pamoja kujifunza pekee yako, katika jozi, katika vikundi vidogo vidogo, au kama sehemu ya timu, na mtu mwenye mamlaka au mtu mzima, na kuwa na shughuli za aina nyingi na zio kurudia rudia (Dunn, R.., Dunn, K., 1989).
Tabia za kisaikolojia ni kigezo kingine cha modeli nyingine ya mtindo wa kujifunza. Ambao unaweza kuathiri kujifunza kwa mwanafunzi. Tabia hii ina maanisha ni lini na kwa vipi mwanafunzi anaweza kujifunza vizuri zaidi. Kuelewa tabia ya mwanafunzi ya kisaikolojia itawasaidia wanafunzi kujifunza kwa kuwatumia uwezo mkubwa. Tabia hii inunganisha masaa ya siku, ushawishi wa nje, nguvu za kujifunza, miondoko wakati wa kujifunza. Kwa mfano mwalimu anaweza kuwashawishi wanafunzi kujifunza wakati mzuri wa siku, ambao unaweza ukawa ni asubuhi sana, kabla hawajaenda shule, wakati wa chakula cha mchana, mara tu baada ya shule, au jioni kabla hawajaenda kulala. Wanafunzi pia wanajibu vingine kwa vishawishi vya nje wanapokuwa wakisoma kwa makini. Wengine wanapenda kula, kutafuna, kunywa, au kuvuta sigara wakati wakijifunza. Licha ya hivyo wanafunzi wengine wanaweza kuwa na nguvu ya kudumu katika enea la uwezo wao au miondoko yao. Wanaweza wakajifunza vizuri au kufanya kazi vizuri wanapokuwa katika madarasa yao kama wanaweza wakawa wanazunguka zunguka wakati wanajifunza na sio kufungia katika sehemu moja ya dawati (Dun, R, & Dunn, K. 1992).
Jinsi wanafunzi wanavyoshughulikia habari inaweza kathiri uwezo wao wa kujifunza. Wanfunzi wengine hujifunza kwa kunyambua habari nao huwa ni wavumilivu. Hawa kwa kawaida hawaanzi kazi zao maramoja, bali mara watakapoanza, huwa na hamukubwa ya kujifunza hazi kazi walizopewa zimemalizika au mpaka wafike mahali watakaposema kuwa sasa imetosha. Wajifunzaji wa kiujumla, kwa njia nyingine hujifunza kwa njia ambayo walimu wa kisasa wanadai kuwa zinawasubua wasielewe.-sauti (misic, kutepu au mazungumzo), muundo wa kawaida (kuanda kwa raha kabisa), mwangaza laini (kufunika macho yao au kuvaa miwani ya ndani), kuelekezana katika jozi (kutaka kufanya kazi na rafiki), kuhitaji chakula (kitafunio) wakati wakisoma (Dunn, R. & Dunn, K., 1992)
Njia nyingine ya kuelemea inaweza kuathiri uwezo wa mwanafunzi kujifunza: kulia/kushoto, kulazimisha au kufikiri. Wanafunzi wengine huelewa habari kwa mfuatano, kwa kunyambua, au kutumia ubongo wa kushoto, kuliko kunyambua kiujumla, au kwa pamoja, au kwa kutumia sehemu ya kulia ya ubongo. Wanafunzi wengine wanaweza kukimbilia kujifunza na kufanya kazi zao kasi sana na alama zao zaweza kuonyesha hii. Hawa wanafunzi wanaolazimisha kujifunza hawatumii muda mwingi sana kujifunza. Mwanafunzi anayefikiria hutumia muda wake ku kufikiria habari, kuelewa madhari amabayo yanafundishwa (Dunn, R., & Dunn, K., 1998)
Kwa nini Modeli ya Mtindo wa Kujifunza
Kwa kutumia modeli ya mtindo wa kujifunza, waalimu wanaweza kujaribu na kujua mtindo wa wanafunzi wa kujifunza kwa uhakika (Beaty, 1986). Kwa mfano, ni vigumu kuamua kuwa mwanafunzi ana harakisha kufanya kazi kutokana na hali ya kuzunguka darasani, au kukaa katika kiti amabacho hakupangiwa, au kwa mambo ya maumbile, au kupumzika, au kutokubaliana na wenzake, au kutokuwa na nidhamu (Shaughnessy, 1998).
Kigezo kimmoja kikubwa cha mwanafunzi kuwa ana ujuzi wao wa kujifunza ni kujiamini.(Martin na pota 1998) sasa wanafunzi hao ambao wako hatarini, wanaonyesha ujasiri na kukubali majukumu yao yakujifunza(Prren 1990 uk 24). Wanafunzi wanapoelewa jinsi ya kujifunza na jinsi ya kujitahidi kujifunza wanaweza wakatawala mazingira yao na kuuliza wanacho kihitaji (Martin na Potta 1998). OBRIEN (1989 ) alisema kwamba labda shule zitumie maandalizi ya mafunzo kuhusu kuinga mitaara (UK85)
Wakati wanafunzi wanaelewa mtindo wao wa kujifunza,hawahitaji kujisikia tofauti kwa sababu wanahitaji utulivu wa kutosha wakujifunza au wanahitaji wanaruhusiwa kuzunguka zunguka darasani (Martin na Potta 1998). Wanafunzi wanaweza wakajifunza somo lolote lile ambalo wamejifunza kwa kutumia mbinu zozote zile na mitindo mbali mbali; wanafunzi wa aina hihiyo hiyo wanaweza wakashindwa kama wamefundisha kwa kijume na uwezo wao (Dunn, R.na 1990 uk 18). De Belo 1996 uk39) Amesema wakuu wa shule na walimu wanawajibu wa kuwafanya wazazi wajue mahitaji ya watoto inayoweza kujifunza katika mazingira Fulani na yanayolingana na mtindo wa uwezo wao.
Labda kitu cha muhimu na watu wa muhimu wanaohitaji kuelewa mitindo inayotumiwa na watoto kujifunza ni wazazi (Guild na Garger, 1985 uk 85). Wazazi wanatakiwa kuelewa tofauti ya watoto wao ili waweze kuwasaidia kuwa kuwa wanafunzi wema (Martin na Potta 1998)
Kuendeleza mafanikio ya wanafunzi
R. Dunn (1998) alihitimisha kuwa wanafunzi hufaulu zaidi kama walimu wao watawafundisha kutokana na mitindo yao ya kujifunza. Hitimisho hili linatokana na minyambuo yamajaribio ya tafiti 42 zilizo fanywa na Dunn na Dunn kuhusu modeli ya mtindo wa kujifunza kati ya mwaka 1980 na 1990 katika vyuo kumi na tatu vya Elimu ya juu. Tafiti hizi zimengundua kuwa wanafunzi ambao tabia zao zilisaidiwa kwa mbinu zilizoandaliwa na waalimu na zilizokuwa zinaendena na mbinu zao za kujifunza walitarajiwa kufauru aslimia 75% ya kiwango cha juu kuliko kiwango cha wanafunzi ambao hawakusaidiwa na walimu wao (R.Dunn kama ilvyo nukuriwa katika Shaughnessy,1998).
Zaidi ya hao watendaji wote wa Marekani wameripoti kuwa kwamba hesaba zinaonyesha kuwa alama kubwa za majaribio au alama za wastani kwa mwanafunzi ambao walitoka katika mafundisho ya jadi na kufundisho ya kutumia mitindo ya wanafunzi ya kujifunzia katika viwango vyote-Secondari, Msingi na vyuo. Kwa mfano Frontier, New York, Elimu muhimu ya wilaya na program yake ilitumia modeli ya kujifunza. Baada ya mwaka mmoja (1987-1988), asilimia ya wanafunzi waliyofaulu iliongezeka kwa asilimia 66 kuliko mwaka uliyo pita. Wakati wa mwaka wa pili (1989-1990) matokeo yalibaki wastani katika asilimia 90%(Brunner na Majewski, ilivyo nukuliwa katika

No comments:

Post a Comment