Wednesday 2 March 2016

TAFSIRI NA MAANA YA HERUFI YA KWANZA LA JINA LAKO


HII NI BENDERA INAYOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA

 MAANA YA HERUFI YA JINA LAKO LA KWANZA



HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu
anayependa mambo makubwa, anajiamini na
mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni
mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na
mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa,
anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda,
HERUFI B
Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu,
mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni
Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale
anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
Herufi B inawakilisha Nyota ya Ngombe,
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu
wa kukubadilika badilika, mshindani na
hupenda kupigania malengo yao wanayopenda.
Ni watu wa wabunifu na wanaopenda
mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya
Mapacha,
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu
anayependa usawa, Biashara. Ni watu
wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda
usafi. Ni jeuri na wenye msimamo. Herufi C
inawakilisha Nyota ya Kaa,
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu
mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na
huruma. mwenye kupenda uhuru katika
mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo
atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
Herufi E inawakilisha Nyota ya Simba,
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu
mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana
uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu
na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya
maamuzi. Herufi F inawakilisha Nyota ya
Mashuke,
HERUFI G
Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu
mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za
kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa
kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia
kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali
ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G
inawakilisha Nyota ya Mizani,
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu
mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,
hupata faida kubwa kutokana na jitihada na
bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo
na mbinafsi. Herufi H inawakilisha Nyota ya
Nge,
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu
mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu.
Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira
za haraka. Herufi I inawakilisha Nyota ya
Mshale,
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu
mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na
muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata
mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa
ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J
inawakilisha Nyota ya Mbuzi,
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu
mwenye jeuri. mwenye msimamo
thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa
kushawishi na kuamsha hisia za watu wana
uwezo wa utambuzi ambao watu wengi
hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.
Herufi K inawakilisha Nyota ya Ndoo,
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa
vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri
kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.
Herufi L inawakilisha Nyota ya Samaki,
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu
mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata
mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka
na mwepesi kukasirika. Herufi M inawakilisha
Nyota ya Punda
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu
mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda
kuwasiliana lakini ana wivu sana. Herufi N
inawakilisha Nyota ya Ngombe
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu
mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya
kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia
jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti
hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu
mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima
kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda
sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu
mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu
wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha
vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza
sana. Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu
mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana
hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda
amani. Herufi R inawakilisha Nyota ya Mashuke
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu
mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu
wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi
makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya
Mizani
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu
mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia
nguvu za ziada kusaidia watu na hupata
mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu
wenye hisia kali sana na ni wepesi
kushawishika. Herufi S inawakilisha Nyota ya
Nge
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu
mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda
uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi,
mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U
inawakilisha Nyota ya Mshale.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu
Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata
hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U
inawakilisha Nyota ya Mbuzi.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu
muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na
mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na
mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya
mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota
ya Ndoo.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu
asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye
anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na
kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya
Samaki.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu
mwenye kupenda Uhuru na hawapendi
kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa
uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika
maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya Punda
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu
mwenye kupenda matumaini na amani. Ni
wenye msimamo mkali ila wanashauriwa
kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z
inawakilisha Nyota ya Ng’ombe