Tuesday 19 April 2016

JE,NI LINI UNAWEZA KUBADILIKA?

Ni muda wako sasa wa kuacha ubabaishaji na kuwa makini
Kama unataka kuanza njia bora na makini katika kazi, usifikirie juu ya kukata tamaa ndani ya mwaka wa kwanza tu. Machache hutokea ndani ya mwaka wa kwanza kutokana na matokeo. Biashara nyingi huwa hazileti faida nzuri ndani ya mwaka wa kwanza; inachukua muda kwa biashara hizo kuwa madhubuti, hata kama ni biashara ndogondogo.

Wengi sana ambao hufanya bloging hukata tamaa miezi 6 tu ya kwanza. Wanakuwa bored, wanapoteza umakini, au kupata wazo bora katika mipango mingine. Unaweza kuwaona wakibadilisha topic zao au majina ya blog zao na wakifanyia kazi mara moja tu kwa mwaka mzima. Baada ya miaka kama mitano hivi kwa aina hii ya ubabaishaji, watakuwa hawajafika kokote. Wakiendelea kufuta hata mpangilio mdogo waliokuwa wameuweka, hivyo hawana nafasi ya kuendeleza jambo lolote la umakini.

No comments:

Post a Comment