Tuesday 19 April 2016

JINSI YA KUTAFUTA WAZO ZURI LA BIASHARA


Wengi huwaza na kuumiza kichwa wanapotaka kuanza biashara zao wenyewe, lakini ni jinsi gani unaweza kupata wazo zuri la biashara ambayo itakusaidia?
Ili kupata wazo zuri ni vema ujue ni nini hasa watu wako wanahitaji, mara nyingi biashara zenye mafanikio huangalia sana mahitaji ya watu waliopo, huwezi kuanzisha biashara tu bila kuwa na wazo. Na sio lazima uwaulize watu wanataka nini. Katika kufanya uchunguzi wako mwenyewe utagundua kitu kinachohitajika na watu unaolenga iwe ni hudum au bidhaa. Read More....

BUSINESS & ENTERPRENEURSHIP | Views: 399 | Author: Yahyou M. Yahya | Added by: Yahya | Date: 14/Jun/2013 | Comments (0)
UFANYE NINI ENDAPO HUIPENDI KAZI YAKO?

UFANYE NINI ENDAPO HUIPENDI KAZI YAKO?
Ukiwauliza watu kadhaa hivi kama wanapenda kazi yao, zaidi ya nusu utasikia hawapendi kazi zao.
Kama huipendi kazi yako, vipi utafanya kazi kwa bidii na kuifanya kazi vizuri?
Kila mtu anahitaji hela, na hivyo, anawajibu wa kufanya kazi ili apate. Hii inamaana kuwa watu wengi sana wanafanya kazi ambazo hawapendi kufanya, na hivyo kutokuwa na furaha katika kazi zao
Kuna watu ambao wanaweza kudiriki kuacha kazi zao na kuangalia njia nyingine, hata kama katika kipindi hicho anakuwa hana njia nyingine ya kumuingizia kipato.
Kuna watu pia, ambao wana imani juu ya uwezo wao na wana ujasiri wa kutafuta kazi, kufanya kile wanachopenda kukifanya.
Kuna watu wenye tamaa kubwa sana, ambao watafanya lolote kuhakikisha wanakamilisha malengo yao.
Lakini vipi kuhusu asilimia kubwa ya watu, ambao huhitaji kufanya kazi, siku hadi siku, siku zote hufanya kile wasichopenda kufanya? Hawawezi na hawataweza kuacha kazi zao na kufanya kile wanachopenda kufanya. Ukweli ni kwamba, sio kila mtu anajua kile anachopenda kukifanya, na kipi kitamfanya awe na furaha na kuridhika nacho. Soma Makala nzima....

No comments:

Post a Comment