FAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU
|
Ubongo wa Mwanadamu |
- Unaweza kuwa umeshawahi kusikia neno SAIKOLOJIA mara nyingi sana,
Lakini hebu tufafanue zaidi kwa yule ambaye hafahamu maana yake. Kwa
kifupi kwanza hili neno ambalo asili yake ni kigiriki likiwa na maana ya
kwamba, saiko ni mambo yanayohusu akili au ubongo, na lojia ni mambo
yanayohusu elimu. Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kwamba saikolojia ni
elimu inayohusu mambo ya akili au ubongo.
- Somo hili la saikolojia
linahusu jinsi wanyama na binadamu wanavyoweza kutumia akili au ubongo
katika kumiliki na kuongoza vitendo na tabia zao.
- Ni wazi kuwa
wanyama wote wana ubongo Lakini ni binadamu peke yake ndiye mwenye uwezo
wa kujifunza kwa kutumia ubongo wake wakati wanyama wengine hujifunza
kwa kutumia silika na mazoea. Na hii humfanya binadamu kuwa tofauti na
viumbe wengine.
- Sehemu kubwa ya saikolojia inahusu jinsi binadamu
anavyoweza kutumia ubongo au akili yake katika kujifunza, kufikiri na
kudhibiti tabia zake.
- Kwa ujumla ni kwamba saikolojia ni taaluma
ya kisayansi inayohusu tabia/mienendo na michakato ya ubongo au akili ya
binadamu katika kujifunza. Tabia au mienendo ni kila kitu ambacho mtu
hufanya na ambacho huweza kuchunguzwa moja kwa moja.
- Tumeangalia kwa ufupi sana maana halisi ya saikolojia, sasa je unaelewa nini kuhusu saikolojia ya elimu?
-
Kuna matawi mbalimbali ya saikolojia kama vile saikolojia ya Elimu,
Saikolojia ya Kliniki, saikolojia ya Biashara, saikolojia ya Kijeshi
n.k. hivyo basi katika mada hii tunaangalia maana ya saikolojia ya elimu
na umuhimu wake.
- Saikolojia ya elimu ni tawi la taaluma ya
saikolojia linaloshughulikia masuala ya elimu, tawi hili linachunguza
jinsi mwanafunzi anavyojifunza mambo mbalimbali ya kielimu, kijamii na
kiutamaduni na namna bora ya kumfundisha. Sasa hebu tuangalie tawi hili
lina umuhimu gani? Au kuna umuhimu gani wa mwalimu kujua saikolojia?
- Umuhimu wa saikolojia ya Elimu
1.Hii humsaidia mwalimu kujua tabia za mwanafunzi na kujua ni kwa njia
au mbinu gani anaweza kuzitumia ili tendo la kujifunza litokee na pia
kujua sababu zinazoweza kufanya tendo la kujifunza lisiimarike mfano
wanafunzi hutofautiana sana kutokana na malezi waliyolelewa au mahala
walipotokea, hivyo kama mwalimu ukishajua tofauti hizi utajua utumie
mbinu zipi ili kuhakikisha kuna usawa wa elimu au ulichokifundisha
kimeeleweka kwa wote bila ya kubagua mwenye uwezo mkubwa au mdogo.
2.Husadia pia kujua jinsi ubongo au akili ya binadamu inavyotumika
katika tendo la kujifunza. Kujua huku kutafufua njia na mbinu mbalimbali
kuhakikisha kinachofundishwa kimefanikiwa.
3.Husaidia kumjua vema mwanafunzi wako na kujua jinsi gani utamsaidia ili ajifunze vema zaidi.
4.Itakusaidia kufahamu matatizo yanayokwamisha mchakato mzima wa
ufundishaji na ujifunzaji na kujua jinsi gani utaweza kuyatatua.
5.Kwa kufahamu saikolojia na tabia za wanafunzi wako utaweza kuwaandaa
vema na kuwapa motisha ili walipende somo na kuwachochea inapobidi.
Mfano unaweza kutumia mifano mizuri ya kile wanafunzi wanachokipenda ili
kuwafanya wawe na furaha na umakini na kile unachokifundisha.
6.Utajua kama mwanafunzi ameelewa au hajakuelewa hata kama amekaa kimya
bila ya kukuuliza au kusema lolote. Kuna wanafunzi huwa na uoga wa
kuuliza swali pale anaposhindwa kuelewa sehemu fulani, hivyo kama una
ujuzi wa saikolojia hali hii unaweza kuigundua kwa wanafunzi wako na
kuirekebisha.
- Kwa upande wangu nina hayo machache, ikiwa una
lolote la kuongezea jisikie huru kuacha maoni yako kwani tuko pamoja
katika kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali.
-
No comments:
Post a Comment