Tuesday 19 April 2016

HASIRA NI NINI NA JINSI YA KUONDOA HASIRA JITAHIDI SIKU ZOTE AKILI YAKO KUFIKIRIA MAZURI NA SIYO KURUHUSU HASIRA



Hasira huja kutokana na hisia za kutoridhika na jambo, msongo wa mawazo na ukosefu wa furaha, ambayo huja sikuzote pale tunapomchukia mtu, kitu au hali fulani.
Hutokea siku zote pale tunaposhindwa kitimiza matakwa yetu, au tunapolazimishwa kufanya kitu ambacho hatupendi kukifanya au ambacho tunaona ni bora kukiepuka. Akili inajawa na ukosefu wa furaha na msongo wa mawazo ambayo mwishowe huleta hasira.
Maisha ya kila siku huwa na hali tofauti ambazo huweza kuleta hasira:
1.Mwenzako, mtoto au rafiki siku zote husema maneno ambayo huyapendi.
2.Unaweza kuchelewa katika kitu cha basi na kukuta gari limekuacha.
3.Unalazimika kuongea na mtu ambaye humpendi
4.Mipango yako hugeuka na kuwa tofauti na ulivyotarajia.
Yote hayo na yanayofanana na hayo huweza kuleta hasira. Swali ni kwamba, je tunalazimika kuwa na hasira au tunaweza kubadilisha matendo yetu ili tuepuke hasira?
Kwa asilimia kubwa sana hasira ni hisia mbaya sana, na inapaswa kuepukana nayo kabisa kama utapenda hasa kujiweka katika njia ya kujiboresha mwenyewe. Huwezi kuepukana na hali zote zinazosababisha hasira, hata hivyo, kw amafunzo fulani unaweza kujifunza kudhibiti na kubadilisha mwenendo wako na tabia. Unaweza kujifunza mwenyewe kuepukana na hasira.
Unahitaji kuwa makini na hali zinazosababisha hasira kuja, na kuwa makini vya kutosha pale unapoona hali hizo zikikujia. Je unataka kuishi kwa kupelekeshwa kama vile Robot? Au unataka kuishi kama mtu mwenye ufahamu kamili na kudhibiti matendo yako? Unaweza kuondosha hasira, lakini hii inahitaji kazi za ndani kabisa na uvumilivu.
1. Ukijihis hauna furaha na faraja, acha kil eunachokifanya kw amuda huo kwanza na anza kufikiria mambo mazuri yanayokupa faraja. Fikiria kitu ambacho kilikuletea furaha hapo nyuma.
2. Ukijihisi kwamba unapatwa na hasira vuta pumzi nzito kama mara tano hivi. Hii inaweza kukawisha hasira na kukupoza.
3. Hesabu taratibu kutoka moja hadi kumi (1 – 10) hii itadhoofisha nguvu ya hasira zako.
4. Katika muda ambao huna kazi, fikiria hasara ya mtu kuwa na hasira na faida zake pale unapoepukana na hasira. Hii itakusaidia sana kujikomaza kifikra kuhusu kuepukana nayo.
5. Kunywa maji. Maji yana pozo fulani ndani ya damu.
6. Jifunze kuboresha uvumilivu na subira. Zifanyie kazi taratibu. Ili uweze kuboresha uvumilivu wako katika mambo mengi hasa yanayokuwa magumu kwako.
7. Moja ya njia bora kabisa ya kuepuka hasira ni kutotilia maanani kila jambo. Ikiwa akili yako haikai na kuumiza kichwa juu ya mambo ya nje yasiyokuwa na faida kwako, huwezi kupata hasira.
Jitahidi kila siku uwe unaizoesha akili yako kufikiria mambo mazuri na sio mambo mabaya na yenye kuhuzunisha. Hii itakusaidia sana kuboresha akili, maisha na afya yako kwa ujumla. Kumbuka kuwa Hasira ni hasara!. Don’t get angry!

 Michael Charles Chali
 Journalist-DSJ
0712562397

No comments:

Post a Comment