Tuesday 19 April 2016

JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA

Hakikisha unaoga kila siku ili kupunguza idadi ya bakteria kwapani kwani husababisha kuweka harufu mbaya kwenye mwili hasa majira ya joto kwa kuwa mara nyingi joto ndilo husababisha jasho na harufu kwapani hivyo unahitaji kuoga mara mbili kila siku, unaweza kutumia sabuni au anti-bacterial na maji ya moto.
Safisha nguo katika maji ya moto na sabuni ya kuondoa uchafu na mafuta, vaa mashati safi. Inapendekeza kuvaa mavazi yenye nyuzi za asili, kama vile pamba na hariri ili kusaidia kunyonya unyevunyevu na kuruhusu ngozi kupumua.
Wakati unafanya mazoezi, tumia nguo zenye vitambaa ambavyo vitanyonya unyevunyevu kwapani ili kuzuia harufu mbaya.
Vinega ‘siki’ na mafuta ya chai ‘ tea tree oil’
Apple cider siki na vinega nyeupe, hupunguza harufu kwapani. Ili kukabiliana na harufu, loweka pamba katika vinega, paka kwenye makwapa badala ya deodorant. Mbali na tiba hiyo, tumia tea tree oil, inaweza pia kuwa na manufaa kwa sababu ni anti-bacterial.
Limao
Kata limao au ndimu nusu kwa kisu. Paka kipande cha limao ulichokata kwenye kwapa lako na hakikisha unalisugua mpaka litoe maji yake. Weka kwapa lako lipate hewa ili hiyo juice ya limao uliyopaka ikauke.
Asidi citric katika maji ya limao inasaidia kutoa tezi ya jasho hivyo kuondoa harufu.

No comments:

Post a Comment