Tuesday 19 April 2016

BORESHA MAPISHI YA NYUMBANI


MALENGO
Moja:Kuboresha mapishi nyumbani
Ingawa Afrika ni Bara lililobarikiwa na vyakula vingi, Ufahamu na ujuzi wa kuandaa chakula Bora chenye ladha nzuri,muonekano wakuvutia na wingi wa virutubisho ni mdogo kwa waafrika wengi.Jiko hili liko hapa kutatua tatizo hili
Mbili:Kuielimisha jamii juu ya virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili.
Elimu ndogo juu virutubisho vya chakula na umuhimu wake katika mwili huwafanya watu wengi wale mlo usio kamili,hivyo kusababisha ukosefu wa virutubisho muhim mwilini na kua chanzo cha magonjwa mbalimbali katika jamii.jiko hili hutoa elimu juu ya virutubisho vya chakula na umuhim wake katika mwili.
Tatu:Kukuza matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa Nchini
Nchi nyingi za Afrika huzalisha bidhaa za chakula. Ingawa bidhaa hizo ni nyingi sana sokoni,watu wengi hupenda kununua na kutumia bidhaa za chakula zitokazo nje.Jiko hili huamasisha waafrika kutumia bidhaa za chakula zinazozalishwa katika nchi zao, kwani bidhaa hizo ni bora na fresh kuliko zile zitokazo nje.Hili litachangia maendeleo na ukuaji wa viwanda vya usindikaji wa vyakula na kukuza uchumi wa nchi za Afrika
DIRA
Dira ya Tollyzkitchen ni kua jiko linalotoa elimu na mafunzo bora ya upishi,chakula na virutubisho,na kuboresha upishi na ulaji wa virutubisho sahihi vya chakula kwa watanzania na watu watumiao lugha ya Kiswahili.Kuona watanzania wakitumia bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini.
DHIMA
•Kutoa Elimu na mafunzo ya upishi,chakula na lishe bora kwa kupitia,tovuti ,simu,redio ,runinga ,vitabu na mafunzo kwa vitendo.
•Kutoa ushauri na maelekezo juu ya chakula na lishe kwa makundi maalum
•Kutoa Elimu juu ya chakula na virutubisho kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ,kwa kushirikiana na taasisi za elimu
•Kufundisha na kuelimisha jamii juu ya upishi,vyakula na lishe bora kwa kutumia michezo,mashindano,muziki na sanaa mbalimbali.
•Kukuza na kuboresha matumizi ya bidhaa za chakula zinazozalishwa hapa nchini kwa kutoa elimu ya uelewa na utambuzi wa bidhaa bora za chakula

No comments:

Post a Comment